August 10, 2014



Huenda mshambuliaji Jerome Ramatlhakwane akaondoka nchini ndani ya leo au kesho kurejea kwao Botswana.
Hali hiyo inatokana na kiwango chake kutowaridhisha mabosi wa Simba kuanzia wale wa kamati ya usajili, hadi bosi wa benchi la ufundi, Zdravko Logarusic.
Loga alimpa Rama dakika 45 katika mechi dhidi ya Zesco, lakini hakuonyesha makeke na mwisho akaishia kuumia.
Taarifa zinasema hakuwa amefanya mazoezi kabla ya kuja nchini, huenda ilichangia kiasi fulani kuonyesha ni ‘bonge nyanya’ na asiye na spidi.
“Nafikiri ataondoka, ila bado ni suala la kusubiri kidogo. Kiongera na Manneh wanaweza kubaki na tutajua baadaye,” kilieleza chanzo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic