Mkurugenzi wa wa Vyama na Masuala ya Kisheria
katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Evodius Mtawala, amelazimika kuachia
ngazi kutokana na sababu mbalimbali.
Taarifa ambazo tumezipata, zinaeleza kuwa
Mtawala ambaye aliwahi kuwa Katibu
Mkuu wa Simba, alikuwa na hali ya kutokuelewana na uongozi wa shirikisho hilo
na ndiyo chanzo kikubwa cha kumfanya ang'atuke TFF.
Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa, alithibitisha
kuachia ngazi kwa Mtawala lakini akasema ni kutokana na sababu mbalimbali za
taaluma yake ya uanasheria.
“Ni kweli Mtawala hataendelea kufanya kazi TFF
lakini ameamua kuchia ngazi mwenyewe kutokana na sababu mbalimbali alizodai
kwamba ni kujikita na taaluma yake zaidi kwa sasa, lakini mambo mengine juu ya
hilo yatabaki kuwa siri baina yake na mwajiri wake.
“Ila mpaka makubaliano ya mwisho yalieleza
kuwa itakapofika mwisho wa mwezi wa nane (jana 31, Agosti) atakuwa tayari
ameshakabidhi ofisi na kuendelea na masuala ambayo alidai anahitaji kujikita
zaidi kulingana na taaluma yake,” alisema Mwesigwa.
Mtawala amedumu kwenye wadhifa huo kwa miezi
nane tu tangu alipoteuliwa Desemba 24, mwaka jana chini ya uongozi wa rais
mpya, Jamal Malinzi.
0 COMMENTS:
Post a Comment