Kocha Mkuu wa Simba, Mzambia, Patrick Phiri,
amesema timu yake itaendelea na kambi kisiwani Unguja hadi itakapocheza mchezo
wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga.
Phiri
alisema timu hiyo itaendelea kuweka kambi ya muda mrefu kisiwani Unguja kwa
ajili ya kujiandaa na michezo ya mwanzoni, ukiwemo dhidi ya Yanga.
Phiri alisema kutokana na ugumu wa mechi hiyo,
timu hiyo haitarejea mapema Dar es Salaam na badala yake itaendelea kupiga
kambi kujiandaa na mchezo huo.
Mzambia huyo aliongeza kuwa, michezo ya kwanza
mitatu ya ligi kuu timu hiyo itaenda Dar es Salaam kucheza mechi zake na
kurejea Zanzibar kuweka kambi kujiandaa na mechi ya Yanga kabla ya kurejea
rasmi.
Aliongeza kuwa, hali hiyo inatokana na ukweli
kwamba anahitaji kukaa na timu pamoja kwa muda mrefu ili kutengeneza kikosi
bora ambacho kitaleta ushindani wa hali ya juu baada ya kukosa mafanikio kwa
muda mrefu.
“Kama
unavyojua timu za Yanga na Simba zinapokutana ushindani huwa ni mkubwa sana,
hivyo timu yangu itaenda Dar es Salaam na kurejea Zanzibar kujiandaa na ligi,”
alisema Phiri.
Phiri aliongeza kuwa, hata kama ikitokea timu
hiyo itapata mechi za kirafiki nje ya Kisiwa cha Unguja, itatoka kwenda kucheza
kisha kurejea tena kisiwani hapa kwa ajili ya kuendelea na mazoezi yake.
0 COMMENTS:
Post a Comment