September 1, 2014



Beki wa kati na nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, ameshangazwa na kitendo cha kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Mganda, Emmanuel Okwi kusaini Simba huku akimwambia: “Tutaonana uwanjani.”
Okwi ametua kuichezea timu hiyo hivi karibuni akitokea nyumbani kwao mara baada ya uongozi wa Yanga kumshtaki kiungo huyo mwenye kasi.
 Cannavaro amesema anashangaa kusikia kiungo huyo kutua Simba akiwa ana mkataba wa miaka miwili ya kuichezea Yanga.
Aliongeza kuwa, hasikitiki na haogopi hata kidogo kuondoka kwa kiungo huyo huku akimtamkia kwamba watajuana vizuri mara watakapokutana uwanjani kama akifanikiwa kuichezea Simba.
“Ujue nilishangaa na kushtushwa juu ya Okwi kusaini mkataba wa kuichezea Simba, ninaona kama filamu ya maigizo kwa kiungo huyo kusaini mkataba akiwa ana mkataba mwingine.
“Nafikiri huyo mchezaji anataka uwe mwisho wake wa kucheza soka, ni maamuzi magumu ameyachukua, lakini katika hilo sitaki niliongelee sana, kikubwa nitaonana na mchezaji huyo ndani ya uwanja mara tutakapokutana,” alisema Cannavaro.

Wakati Cannavaro akisema hayo, Okwi mwenyewe amewaahidi ubingwa wa Ligi Kuu Bara mashabiki wa Simba.
“Ninajua mashabiki wa Simba wana kiu ya ubingwa wa ligi kuu, hivyo waondoe hofu mara baada ya kurejea kwenye klabu niipendayo kutoka moyoni.
“Niliichezea Yanga kwa maslahi, lakini siyo mapenzi kutoka moyoni, hivyo mashabiki watarajie mengi kutoka kwangu,” alisema Okwi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic