Chelsea imeshindwa kufurukuta nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya mabao 1-1 dhidi ya Schalke 04 katika mechi iliyochezwa nyumbani Stamford Brigde, London.
Juhudi za Jose Mourinho kufanya mabadiliko kadhaa hazikuzaa matunda na bao pekee la Cesc Fabregas lilibaki huku Schalke wakisawazisha na kufanya mambo yawe magumu kwa Chelsea.
Jerome Boateng ambaye aliwahi kuwa beki wa Man City, leo ameibuka kuwa shujaa wa Bayern Munich baada ya kufunga bao pekee katika dakika ya 90.
Huku ikionekana kama mechi hiyo ndani ya Dimba la Alianz Arena utamalizika kwa sare, Boateng aliyecheza beki tano, alimaliza kazi na kuizamisha City.
Barcelona nayo ikiwa nyumbani, ikaibuka na ushindi kiduchu wa bao 1-0 tu lililofungwa na Gerard Pique kwa kichwa.
Mechi hiyo dhidi ya Apoel ilionekana itakuwa njanja kwa Barcelona, lakini ililazimika kufanya kazi ya ziada na kushinda kwa bao hilo moja.
Gervinho raia wa Ivory Coast naye akaibuka shujaa kwa kuingoza AS Roma kuivuruga CSKA Moscow ya Russia kwa mabao 5-1, yeye akitupia mawili.
MATOKEO MENGINE:
Porto 6-0 BATE Borisov

Athletic Bilbao 0-0 Shakhtar
Ajax 1-1 PSG
Maribor 1-1 Sporting
0 COMMENTS:
Post a Comment