Hatimaye Yanga imekubali kuilipa FC Lupopo fedha dola 15,000 kwa ajili ya mchezaji Mbuyu Twite.
FC Lupopo ya DR Congo ililalamika kwamba Yanga ilikiuka mkataba kwa kuingia mkataba na Twite.
Awali mmoja wa viongozi wa FC Lupopo, Constantine Kabika alisema wanakwenda kwenye Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kuliwasilisha suala hilo.
Lakini leo, Yanga imethibitisha kwamba italipa fedha hizo.
Lupopo ilisema Twite ni mchezaji wake na Yanga ilimchukua kwa mkopo kwa miaka miwili na kama inataka kuingia naye mkataba ni lazima iilipe Lupopo.
Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu amethibitisha Yanga kuwa italipa fedha hizo.
"Kweli tumezungumza na uongozi wa Lupopo, hivyo tutawalipa na kumalizana nao.
"Lakini tunataka utaratibu ufuatwe, mfano kuandikishana na kuhakikisha kuwa tumelipa fedha ili kuwe na kila kitu kiwe wazi. Kifupi utaratibu mzuri," alisema Njovu.
Awali Yanga ilisema haikuwa inadaiwa, lakini baada ya kuupitia mkataba uliokuwa umeandikwa Kifaransa, ikaonekana kugundua jambo hilo.
0 COMMENTS:
Post a Comment