Simba imepata pigo jingine baada ya beki wake wa
pembeni mkongwe, Nassor Said ‘Chollo’ kuumia mkono wa kulia wakati timu yake
ilipocheza dhidi ya Polisi Morogoro juzi, hivyo kuna uwezekano wa kuikosa mechi
dhidi ya Yanga.
Tayari Mkenya, Paul Kiongera na kipa Ivo
Mapunda wataikosa Yanga kutokana na majeraha. Simba itakutana na Yanga Oktoba
18 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Vipimo vya madaktari atakavyofanyiwa leo,
ndiyo vitaamua hatma yake ya kuikosa mechi ya Yanga.
Chollo alipoumia juzi, alilazimika kufungwa bandeji
na kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na William Lucian ‘Gallas’.
Daktari
Mkuu wa Simba, Yassin Gembe, alisema hatima ya beki huyo itajulikana baada ya
vipimo vya mwisho atakavyovifanya leo kwenye Hospitali ya Mkoa wa Temeke.
Gembe alisema, bado haijulikani beki huyo
amepata tatizo gani kwenye mkono huo wa kulia kama ameteguka au kuvunjika,
hivyo hatima yake itajulikana leo.
“Hivi
sasa anaendelea kupata matibabu ya timu kutoka kwangu na kesho nitampeleka
kwenye Hospitali ya Mkoa wa Temeke kwa ajili ya vipimo zaidi ili kujua amepata
majeraha gani kabla ya kutoa tamko rasmi kuwa atakuwa nje ya uwanja muda gani,”
alisema Gembe.
0 COMMENTS:
Post a Comment