BENZEMA AKIPACHIKA BAO LA 1000... |
Klabu ya Real Madrid imekuwa ya kwanza
kufunga mabao 1000 katika michuano ya Ulaya.
Mshambuliaji wake Karim Benzema raia wa Ufaransa
ndiye aliyefunga bao hio la 1000 wakati Madrid ikishinda mabao 5-1 dhidi ya
Basle ya Uswiss katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi.
Benzema ameingia kwenye rekodi za klabu hiyo
kwani wa mwisho alikuwa ni Cristiano Ronaldo ambaye alifunga bao la 900 mwaka
2011 wakati Madrid ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Lyon.
Mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Roberto
Soldado ndiye alifunga bao la 800 akiunganisha krosi ya David Beckham.
Lakini kabla ya Soldado, mshambuliaji nyota
zaidi wa klabu hizo enzi hizo, Raul Gonzalez ndiye alipata rekodi ya kufunga
bao la 700.
Alifunga bao hilo siku ambayo alikuwa
ameweka rekodi ya kufikisha mabao 71 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
0 COMMENTS:
Post a Comment