Kipa
namba moja wa Simba, Ivo Mapunda amemuonya kiungo wao mshambuliaji, Mganda,
Emmanuel Okwi, kuwa asiwajibu na wala kuwafikiria mashabiki wa Yanga kila
wanapomzomea akiwa ndani na nje ya uwanja.
Ivo
ambaye amewahi kuichezea Yanga, aliitoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache tangu
itangazwe rasmi na Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwa Okwi yupo huru kuichezea Simba.
Okwi,
hivi karibuni alisaini mkataba wa miezi sita ya kuichezea Simba kabla ya Yanga
kumshtaki TFF ikitaka imlipe fedha za usajili ilizompa huku ikimuondoa kwenye
usajili wa msimu ujao.
Ivo
amesema zomeazomea ya Yanga isimchanganye kabisa Okwi, kikubwa anachotakiwa ni
kufanya kazi yake ndani ya uwanja.
Ivo
alisema Yanga wanafanya kitendo hicho kwa ajili ya kumchanganya kisaikolojia
ili asicheze soka, sasa yeye akizisikiliza kelele zao basi soka litamshinda.
“Katika
maisha siyo kila mtu anakupenda, ni vyema kwanza Okwi akalifahamu hilo,
anachotakiwa kukifanya ni kuachana na mashabiki wa Yanga pale wanapomzomea
anapokuwa uwanjani kwa kuweka pamba masikioni na kucheza soka.
“Lakini
kama akitaka kujibizana nao, basi hatacheza soka tena na asipoangalia atashusha
kiwango chake, mimi niliongea kabla ya mechi ya kirafiki na Gor Mahia nikijua
lazima hali hiyo itatokea,” alisema Ivo.







0 COMMENTS:
Post a Comment