KISIGA AKIWA KAZINI... |
Kiungo wa Simba, Shabani Kisiga, amesikitishwa
na kitendo cha kumkosa kiungo mwenzake Paul Kiongera na juzi Jumamosi alimwaga
machozi hadharani mbele ya kocha wake, Patrick Phiri.
Kisiga, aliyetua Simba akitokea Mtibwa Sugar,
anaamini kama Kiongera angekuwepo kwenye kikosi cha Simba kwa sasa, safu yao ya
ushambuliaji ingekuwa na makali yasiyozuilika. Kiongera atakuwa nje ya uwanja
kwa zaidi ya wiki nane akisumbuliwa na goti.
Simba tayari imeshapata sare mbili katika michezo miwili ya mwanzo kwenye Ligi Kuu Bara ikiwa imejikusanyia pointi mbili tu.
Mkongwe huyo
alisema ingawa kikosi hicho kina wachezaji wengi, anaumia kuona wachezaji
wenzake wanapata majeraha mapema.
“Kutupwa
nje kwa Kiongera si jambo zuri lakini hatuwezi kuzuia, ni kwa sababu ya
majeraha, tulitamani kuwa naye lakini bado kuna wachezaji wengi ambao wataziba
nafasi yake hiyo,” alisema Kisiga.
Juzi Jumamosi Kisiga alitokwa na machozi mbele
ya Phiri baada ya Simba kulazimishwa sare na Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar.
Alipoulizwa baadaye, kiungo huyo ambaye ni
mtaalamu wa kupiga pasi zenye macho, alisema: “Mtu yeyote mwenye kutaka
mafanikio pindi mambo yake yanapokwenda ndivyo sivyo lazima aumie, hali hiyo
ndiyo niliyonayo mimi kwa sasa.
“Natamani kuiona Simba safari hii inafanya
vizuri lakini mambo yakuwa magumu, sijui ni kwa nini lakini sina jinsi, inabidi
nikubali matokeo.”
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment