Kocha Mkuu wa Ujerumani,
Joachim Loew alitumia karibu dakika nzima akizungumza na kumpongeza beki Marcos
Rojo wa Argentina.
Loew ambaye ameipa
Ujerumani ubingwa wa dunia kwa kuifunga Argentina bao 1-0 nchini Brazil, hivi
karibuni, alionekana kufurahishwa na Rojo katika mechi hiyo ya kirafiki.
Kocha huyo alimpa mkono
Rojo aliyejiunga na Man United na kuzungumza naye maneno kadhaa huku
akiutingisha mkono wake.
Katika mechi hiyo ya
kirafiki, Ujerumani ililala kwa mabao 4-2.
0 COMMENTS:
Post a Comment