Kocha Arsene Wenger ameeleza wazi kuwa
ataendelea kumfukuzia kwa kasi kipa Iker Casillas wa Real Madrid wakati wa
dirisha dogo la usajili Januari, mwakani.
Tayari Wenger alionyesha nia yake ya kumpata
Casillas ambaye amekaa Madrid kwa zaidi ya miaka 14 sasa.
Casillas anaonekana kutokuwa na furaha
Madrid na hivi karibuni mashabiki walimzomea.
Lakini Wenger pia anaonekana hafurahii kwa
asilimia mia kazi ya kipa wake namba moja Wojciech Szczesny ambaye alikuwa
langoni walipochapwa 2-0 na Borussia Dortmund, usiku wa kuamia leo.
Bado haijajulikana kama Madrid itakuwa
tayari kumuachia Casillas, lakini Wenger anaonyesha ataendelea kuweka wazi nia
yake.
0 COMMENTS:
Post a Comment