Kocha Mkuu wa Yanga, Mbrazili Marcio Maximo,
ameibuka na kusema kuwa kwa sasa hatashiriki katika uigizaji kama alivyofanya
miaka ya nyuma.
Maximo
amesema kipindi kile alipata fursa ya kuigiza kwa kuwa alikuwa ana muda wa
kufanya hivyo kwa kuwa majukumu ya Stars yalikuwa hayabani sana.
“Kipindi
kile nilipata likizo ya wiki moja na nilipofuatwa na Bongo Muvi wakitaka
niigize, nikaona si vibaya kuwakubalia ombi lao na tukafanya kazi.
“Kwa sasa nina mambo mengi ndani ya Yanga kwa
hiyo sina muda wa kufanya tena kama vile lakini ninafurahi jinsi Bongo Muvi
wanavyonikubali na mimi nafurahia pindi ninapoona mafanikio yao,” alisema
Maximo.
0 COMMENTS:
Post a Comment