Mshambuliaji Paul Kiongera
hajui achukue jezi gani kwa kuwa haitaki ile namba 5 aliyokuwa akivaa Donald
Musoti ambaye ameachwa na Simba.
Musoti amesisitiza alikuwa
akitaka kupea jezi namba 29 ambayo anaitumia Miraji Adam.
“Bado naona namba 29 ni
nzuri kwangu, Simba natakiwa kutumia namba 12, lakini sioni kama
inanifurahisha.
“Nitazungumza nao zaidi na
kujua kama inawezekana kupata nyingine, au nitachukua itakayopatikana,”
alisema.
Kiongera tayari ameungana
na Simba kwenye kambi ya Zanzibar na kuanza mazoezi.
Mshambuliaji huyo wa zamani
wa KCB pia anakipiga katika kikosi cha timu ya taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’.
0 COMMENTS:
Post a Comment