Timu ya Ndanda FC imeonyesha imepania kufanya vizuri kwenye Ligi
Kuu Bara baada ya kuimakamata Simba na kutoka nayo sare ya bila kufungana.
Katika mechi iliyochezwa leo kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini
hapa.
Mechi hiyo ilikuwa ni ya ushindani huku Ndanda ikionyesha soka la
kuvutia na kushangiliwa muda mwingi.
Hata hivyo, Simba ambayo ilianza bila ya wachezaji wake akiwemo
Okwi aliyekuwa benchi, ilibadilika katika kipindi cha pili na kucheza soka la pasi
nyingi.
Ndanda walifanikiwa kuzitikisa nyavu za Simba katika dakika ya 57
kupitia Jacob Masawa lakini mwamuzi akasema mfungaji alikuwa ameotea.
Baadaye Okwi aliingia na kuzidi kuifanya Simba kupata kasi, lakini
mabeki wa Ndanda walikuwa imara.
Mwenyekiti wa Simba, Evans Aveva na yule wa zamani wa klabu hiyo,
Hassan Dalali walikuwa kati ya waalikwa katika mechi hiyo ambayo ilikuwa ni
maalum Ndanda Day.
Kikosi cha Simba leo.
Casillas, Chollo, Abdi Banda, Abdulaziz Makame,Joram Mngeveke,
Said Hamis, Ibrahim Twaha, Amissi Tambwe, Abdallah Seseme,Ibrahim Ajib na
Ramadhani Singano ‘Messi’.
0 COMMENTS:
Post a Comment