Kocha Patrick Phiri raia wa Zambia amesema
unatakiwa umakini mkubwa wa zaidi ya asilimia 100 kukiendesha kikosi cha Simba.
Phiri raia wa Zambia amesema Simba ina
kikosi kipana ambacho kinaweza kumchanganya kocha yoyote asiye makini.
“Kuna wachezaji wengi sana wenye vipaji vya
hali ya juu, wako walio tayari, wako wanaotakiwa kusaidiwa, kupikwa ili
wacheze.
“Hawa wote wako Simba, ili kupata watu 11
wanaocheza inatakiwa umakini wa juu na utulivu.
“Kingine kizuri ni kila mmoja anajituma na
anatambua ushindani uliopo hapa (Simba), si kazi lahisi,” alisema Phiri katika
mahojiano na SALEHJEMBE.
“Ninaamini mimi na wasaidizi wangu tunalijua
hilo, hivyo tutajihidi kufanya uamuzi sahihi kulingana na wakati sahihi.”
Simba ina wachezaji zaidi ya watano wenye
uwezo wa kucheza zaidi ya namba nne uwanjani.
Pia ina wachezaji watatu katika kila namba,
hali inayofanya ushindani kuwa mkali ndani ya kikosi hicho.
0 COMMENTS:
Post a Comment