MWENYEKITI WA KAMATI YA SHERIA YA YANGA, SAM MAPANDE (KULIA) AMBAYE ALIIWAKILISHA YANGA KWENYE KAMATI YA SHERIA NA HADHI YA WACHEZAJI YA TFF ILIYOAMUA JANA EMMANUEL OKWI NI HURU KUICHEZEA SIMBA. |
Uongozi wa klabu ya Yanga umesema utapinga maamuzi ya kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji kuhusiana na maamuzi yake ya kumtangaza mchezaji wake, Emmanuel Okwi kuwa huru.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Sheria ya Yanga, Sam Mapande amesema kuwa hawajaridhishwa na
maamuzi hayo ambayo yanakinzana na sataka zima la mchezaji huyo.
Mapande
alisema kuwa kamati ya TFF imeamua sakata la Okwi kinyume na malalamiko yao
kwani hakukuwa na lalamiko la mchezaji huyo wa Uganda kuhusiana na malipo ya
fedha zake za usajili.
Alisema
kuwa cha kushangaza, kamati hiyo ya TFF iliamua kusikiliza kesi ambayo haikuwa
mbele yao na kutoa maamuzi ambayo hata wao wameshangazwa nayo.
“Kwanza
kesi yenyewe ilikuwa haijamalizika, walituambia tuwasilishe vielelezo kuhusiana
na kitendo cha mchezaji huyo kufanya mazungumzo na klabu ya Misri, lakini cha
kushangaza maamuzi yametolewa, hili limetushangaza sana,” alisema Mapande.
Alisema
kuwa mazingira yalikuwa yameandaliwa kuibeba Simba na Okwi kwani hata
malalamiko yao kwa Simba hayakusikilizwa. “Malalamiko yetu yalikuwa wazi
kabisa, yapo kimaandishi, hatukuwai kulalamikiwa, suala la fedha za usajili la
Okwi limetoka wapi, kama lilikuwepo, mbona hatujajulishwa kimaandishi kama
utaratibu ulivyo,” alisema.
Alisema
kuwa Kamati hiyo kumruhusu mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo Zacharia Hans Pope
ambaye pia ni mwenyekiti wakamati ya usajili ya Simba kuwemo katika kikao hicho
kinyume na taratibu za Fifa kupitia kifungu namba 19 kinachoeleza mgongano wa
kimaslahi.
Yanga wanachekesha sana. Kamati yenu ya sheria ndo inafikiria madudu hivi, au ndo mfa maji.... Sasa kama kisheria mkataba wenu na Okwi ulishavunjika kwa kushindwa kutekeleza kipengele namba 8 cha mkataba, mnataka hayo madai yenu mengine dhidi ya Okwi yasikilizwe kwa msingi upi? Hamkuwa tena na uhusiano wa kimkataba na Okwi wakati mnapeleka malalamiko yenu.
ReplyDeleteSijui mchezaji wetu kaongea na klabu ya Misri wakati akiwa na mkataba, kasaini simba akiwa na mkataba na Yanga, sijui hajamtumikia mwajiri wake Yanga hivyo tunamdai fidia na kutaka mkataba uvunjwe. Haya madai yote hayawezi kusikilizwa, kwa sababu huo mkataba mnaoungelea haupo, mlishauvunja wenyewe jamani tusichoshane, msiwachoshe TFF wala FIFA.
kwakweli Yanga imekula kwenu
ReplyDelete