Mshambuliaji
nyota wa Barcelona, Leo Messi ametua mjini Milan, Italia na kula ‘mibata’.
Messi
amewasili Milan akiwa na mpenzi na mzazi mwenzake, Antonella Rocuzzo na
kutembelea sehemu mbali za mji huo.
Baadaye Messi
ambaye amepata ruhusa kutoka kwa Kocha wa Barcelona, Luis Enrique kula ‘mibata’
alikula chakula cha usiku katika hoteli moja ya kifahari.
Katika
chakula hicho cha usiku, pamoja na Messi wake, mmiliki wa kampuni kubwa ya
mitindo duniani ya Dolce&Gabanna ambayo inamdhamini Messi alijumuika nao.
Messi ambaye
alikuwa majeruhi, tayari amepewa taa za kijani kuivaa Athletic Club wikiendi
hii.
0 COMMENTS:
Post a Comment