Nahodha wa Chelsea, John
Terry ameisaini jezi yake ya mechi na kuituma kwa mmoja wa mashabiki wa Chelsea
aliyefiwa na mama yake.
Shabiki huyo alitumiwa
ujumbe na Terry kupitia mtandao wa kijamii akimuambia kuwa amemtumia zawadi
hiyo ya jezi kumfariji.
Terry aliandika: Pole sana
taarifa za majonzi kuwa mama yako amefariki dunia.
Ningependa kutuma moja ya
jezi zangu kwa ajili ya mechi na kuweka saini yangu ili ujue mimi na Chelsea
tuko pamoja nawe katika kipindi hiki kigumu.
Baadaye shabiki huyo
aitwaye Louise alituma kwenye Instagram akionyesha jezi hiyo baada ya kuipokea.
0 COMMENTS:
Post a Comment