CHANONGO (KULIA) AKIPAMBANA |
Baada ya Simba kuwa na
uhakika sasa itamkosa mshambuliaji wake Paul Kiongera katika mechi dhidi ya
Yanga, sasa mwingine tena, Harun Chanongo ataikosa mechi ya Jumamosi.
Simba inashuka dimbani
Jumamosi kuwavaa Stand United ya Shinya.
Taarifa zinaeleza, Chanongo
ataanza mazoezi mepesi Alhamisi au Ijumaa, hivyo itakuwa vigumu kucheza mechi
ya Jumamosi.
Hivyo kocha Patrick Phiri
atalazimika kumtumia mchezaji mwingine, huenda nafasi hiyo akaichukua mkongwe
Amri Kiemba.
Chanongo pia aliumia katika
mechi dhidi ya Coastal Union na anatakiwa kupumzika siku nne.
Uhakika unaeleza itakuwa
vigumu kuwavaa Stand kutokana na maumivu aliyokuwa nayo kuhitaji mazoezi ya
taratibu angalau siku nne nyingine.
0 COMMENTS:
Post a Comment