September 5, 2014


Kiungo mshambuliaji wa Thika United ya Kenya, Moses Odhiambo ameukataa uwezo wa mshambuliaji wa Yanga, Genilson Santana 'Jaja' lakini akasema Andrey Coutinho ni mtu hatari.


Odhiambo aliyewahi kuzitumikia Simba na Yanga, ameliambia gazeti hili kuwa, wachezaji hao raia wa Brazil wanaweza kupata wakati mgumu kucheza soka la Tanzania lakini akasema angalau Coutinho anaweza kuwa mchezaji muhimu.

Odhiambo, raia wa Kenya ambaye alikuwa nchini na kikosi chake kilichofungwa na Yanga bao 1-0 katika mechi ya kirafiki kwenye Uwanja wa Taifa jijini, juzi amenukuliwa akisema:

“Unajua yule Jaja ingawa ametufunga lakini hataweza kuimudu hii ligi ya Tanzania, ligi ya hapa ni ngumu na yeye si aina ya wachezaji wa kupambana kama washambuliaji wengine niliowahi kuwaona, kwanza atachoka haraka kutokana na mabeki atakaokwenda kukutana nao.

“Yaani ukiiangalia Yanga kote imekamilika lakini tatizo lipo pale mbele anapocheza huyo Jaja, labda kama Yanga inataka kufanya kweli wafanye juhudi za kuwarejesha kwenye viwango vyao Jerry Tegete na (Said) Bahanuzi maana nasikia siku hizi hawako vizuri kama mwanzo.

“Yule Coutinho ni mchezaji mzuri, ana chenga na anajua kuuchezea mpira lakini hana nguvu za kutosha, halafu hataweza kuisaidia Yanga kwa sababu ni mtu wa kupiga chenga kwa ajili ya faida ya mashabiki na si kwa ajili ya timu yake.”




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic