Simba imeendelea na
mazoezi leo kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya watani wake
Yanga, Oktiba 18 jijini Dar es Salaam.
Mazoezi hayo ni sehemu ya
kujiweka vizuri kabla ya mechi yake ya kwanza ya kirafiki dhidi ya Orlando
Pirates ya Afrika Kusini.
Mechi hiyo itakayopigwa
kwenye kitongoji chenye weusi wengi cha Soweto jijini Johannesburg, itakuwa ni
ya kwanza kwa Simba.
Taarifa zinaeleza Simba
itacheza mechi mbili ingawa keshokutwa Jumamosi, itawakosa wachezaji wake walio
katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars ambayo itakuwa inacheza na Beni
jijini Dar.
Wachezaji wake walio
Stars ni Joram Mgeveke, Jonas Mkude, Said Ndemla, Amri Kiemba na Haruna
Chanongo ambao watatua Johannsburg maarufu kama Jozi, Jumatatu.
Simba pia itamkosa Okwi
ambaye atabaki Kampala, Uganda akiitumikia timu yake ya taifa inayotafuta
nafasi ya kucheza Kombe la Mataifa Afrika.









0 COMMENTS:
Post a Comment