Bondia nyota duniani, Floyd
Mayweather amesema baba yake amekuwa akimueleza apigane na Mwingereza Amir Khan
na kumziba mdomo.
Mayweather ana matumaini
makubwa kutakuwa na pambano kati yake na Khan raia wa Uingereza.
Baada ya Mayweather kumpiga Marcos Maidana kwa mara ya pili,
swali limekuwa atapigana na nani.
Mani Paquiao na Khan ndiyo
walikuwa wakipewa nafasi ya kuzichapa na mkali huyo.
Hata hivyo inaonekana Khan
ndiye ameshinda nafasi hiyo ya kucheza na Mayweather ambaye amepigana mara 47 bila ya kupoteza.









0 COMMENTS:
Post a Comment