October 12, 2014

 Kocha wa Toto African ya Mwanza, John Tegete ameamuambia Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, daima huwa hafurukuti mbele yake.


Tegete ambaye ni Baba wa mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete alimuambia Julio maneno hayo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa baada ya Toto kuilaza Mwadui kwa bao 1-0 katika mechi ya Ligi Daraja la Kwanza, jana.
Tegete alionekana mwenye furaha baada ya mechi hiyo iliyokuwa na ushindani wa juu.
Akamfuata Julio, akamkumbatia na kuanza kutoa tambo zake.
Hata baada ya kuachana na Julio, Tegete aliendelea kutamba: “Julio ni mdogo wangu, anajua kwangu huwa hafurukuti.”
Hata hivyo makocha hao wawili walionyesha ukongwe ikiwa ni pamoja kuzungumza kabla na baada ya mechi huku kila mmoja akionyesha utulivu kabla na baada ya mechi.
Mechi hiyo ilihudhuriwa na mashabiki wengi, ingawa baadhi ya mashabiki walionekana si waelewa, wapenda sifa bila ya kuzingatia umri mkubwa walionao wakitaka kulazimisha kupigana na wenzao, hali iliyoonyesha hawajitambui na huenda upungufu wa kutopata nafasi ya kuhudhuria mechi kwenye viwanja vingine vikubwa, ili waweze kijifunza.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic