Beki wa zamani wa Simba, Victor Costa ‘Nyumba’,
amejikuta akiingia katika hasara kubwa baada ya nyumba yake iliyopo Tegeta
jijini Dar, kuteketea yote kwa moto usiku wa kuamkia jana Jumanne.
Masaibu hayo yamemkuta Costa wakati
yeye akiwa mkoani Shinyanga na timu yake ya sasa ya Mwadui FC.
Costa amesema chanzo cha moto huo ni kibatari kilichowashwa baada ya umeme
kukatika na baadaye moto wa kibatari kushika kwenye pazia na kwa kuwa watu
hawakuwepo ndani, moto ule ulisambaa.
Costa aliongeza kuwa moto huo
umeteketeza kila kitu kilichokuwa ndani ya nyumba na hakuna kilichosalimika.
“Moto umesababishwa na moto wa
kibatari ulioshika pazia na baadaye kusambaa nyumba nzima, kulikuwa hamna mtu
hivyo haukuzimwa kirahisi.
“Hakuna
kitu kilichookolewa, moto umeteketeza kila kitu kilichokuwa ndani ya nyumba
yangu,” alisema Costa.








0 COMMENTS:
Post a Comment