Wachezaji wa Yanga wameanza kujiandaa
jinsi ya kushangilia mabao watakapocheza mechi ya Watani wa Jadi dhidi ya Simba
katika Uwanja wa Taifa, Oktoba 18.
Yanga na Simba watakutana katika
mchezo wa Ligi Kuu Bara, huku Yanga ikiingia na historia ya kushinda michezo
miwili kati ya mitatu ya ligi hiyo na Simba
ikiwa bado haijapata ushindi wowote
lakini haijafungwa.
Katika mazoezi ya Yanga, viungo
washambuliaji, Haruna Niyonzima na Simon Msuva, ndiyo waliokuwa vinara wa kufanya
zoezi hilo maalum la jinsi ya kushangilia mabao ambayo wataitandika Simba
katika mtanange huo ambao umesalia siku kumi upigwe.
Viungo hao walitengeneza staili ya
kukimbia katika kona ya uwanja na kujichezesha mabega huku mkono mwingine ukiwa
kwenye mapaja. Wachezaji wenzao, Hassan Dilunga, Kelvin Yondani na Mrisho
Ngassa walionyesha kuipenda hiyo staili huku wakifurahi jinsi Msuva na
Niyonzima walivyoicheza.
Mechi ya Simba na Yanga ndiyo kubwa
zaidi kuliko zote hapa nchini na imekuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa sana na
mashabiki.







0 COMMENTS:
Post a Comment