October 25, 2014


Beki kisiki na nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amemshukuru Kocha Hemed Morogo kumteua kwenye kikosi cha Zanzibar Heroes.

Cannavaro ambaye amekuwa akiendelea kupaa kwa kiwango kizuri, amesema Morocco amempa moyo kwa kuonyesha kudhamini mchango wake.
“Najisikia faraja, pia namshukuru Morocco kwa kuuona mchango wake kuwa unahitaji kwenye timu yangu.
“Najisikia faraja, nasikia nina deni la kuwalipa Wazanzibar,” alisema Cannavaro ambaye sasa yuko na Yanga mkoani Shinyanga wakijiandaa leo kuivaa Stand United.

Beki huyo na wenzake Aggrey Morris na Mwadini Ally waliondolewa kwenye kikosi hicho na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Salum Bausi baada ya kugawana fedha za zawadi za ushindi wa tatu kwenye michuano hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic