Dereva Taxi mjanja wa nchini Saudi Arabia, amefanikiwa kupata picha ya pamoja na mshambuliaji mwenye vituko wa Barcelona, Luis Suarez.
Kijana huyo ambaye jina lake halikutambulika mara moja, alifanikiwa kupata picha hiyo haraka bila ya Suarez kung'amua wakati akiwa amembeba kwenye taxi yake.
Suarez yumo nchini humo kwa ajili ya mechi ya kirafiki ambayo Uruguay itawavaa wenyeji wao.
Nyota wengi wamekuwa hawapendi kupigwa picha hadi wanapotoa ruhusa yao.








0 COMMENTS:
Post a Comment