Kocha wa Makipa wa Klabu ya Simba, Zdravco
Djekic, amesema foleni za Dar es Salaam zimekuwa zikimchosha na kumchanganya
akili akihofia kuchelewa kushindwa kukamilisha programu zake za mazoezi.
Kocha huyo mgeni nchini, ni raia wa Serbia
aliyekulia Afrika Kusini, amekuwa akiinoa Simba tangu Oktoba 10, mwaka huu
wakati Simba ilipokwenda Afrika Kusini.
Kocha huyo
alisema hajawahi kuishi kwenye jiji lenye foleni kama Dar, hivyo kukaa kwa muda
mrefu kwenye foleni kunamfanya achoke na kumvuruga akili kitu ambacho siyo
kizuri kwa kocha.
“Foleni za Dar zinanitisha sana, naogopa nisije
siku nikafika wakati muda wa kumaliza mazoezi umefika. Tunakaa sana barabarani
hadi mtu unachoka, ikiwa nitaishi karibu na uwanja wetu tunaofanyia mazoezi
nitafurahi sana,” alisema Djekic.
0 COMMENTS:
Post a Comment