Wakati timuatimua ikiendelea ndani ya Ndanda
FC, kutokana na mwendo mbovu wa timu, zimeibuka taarifa kuwa sababu kubwa ya
kufanya vibaya ni mgogoro wa viongozi ndani kwa ndani na wachezaji kutolipwa
stahiki zao.
Taarifa hizo zimeibuka siku chache baada ya
aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Denis Kitambi na Katibu Mkuu, Edmund Njowoka
kutimuliwa.
Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinadai
viongozi kwa sasa wapo bize kushughulikia migogoro huku wachezaji wakiwa katika
hali ngumu kwa kutolipwa mishahara.
“Jambo baya zaidi ni kuwa, bado kuna wachezaji
wanaidai klabu fedha zao za usajili ambazo hawajamaliziwa mpaka leo, ndiyo
maana wamekuwa wakicheza chini ya kiwango,” kilisema chanzo.
Katibu Msaidizi wa Ndanda, Suleiman Kachele,
alipoulizwa juu ya tuhuma zote hizo, alisema siyo kweli.
0 COMMENTS:
Post a Comment