Jumla ya wanachama na mashabiki 35 wa Klabu ya
Yanga kutoka matawi ya Tandale Kwa-Mtogole na Mpira Akili, wametenga shilingi
milioni mbili kwa ajili ya kuifuata timu yao mkoani Shinyanga katika mchezo
dhidi ya Stand United.
Katibu wa Tawi la Mpira Akili, Abass Ngau,
ameliambia Championi Ijumaa, jana kuwa walitarajia kuondoka leo Ijumaa alfajiri
kwenda Shinyanga ambapo amesema huo ndiyo utaratibu waliojiwekea kwa ajili ya
kuipa sapoti timu yao ambayo ina nyota kadhaa akiwemo Mbrazili Andrey Coutinho.
“Tupo kama watu 35 na kila mmoja amechanga
shilingi 70,000, huo ni utaratibu ambao tumejiwekea ili kuongeza hamasa kwa
timu yetu na pia watu wa Tawi la Tandale wametuunga mkono,” alisema Abass.
Yanga itakuwa mgeni wa Stand, kesho Jumamosi
katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment