Kocha
Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo, amemuongezea majukumu ya uwanjani kiungo wake
mshambuliaji, Andrey Coutinho kwenye kikosi chake.
Mchezaji
huyo ambaye alikuwa majeruhi kwa muda, alirejea hivi karibuni na kucheza mechi
ya kwanza ya ligi kuu dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam baada ya kupona majeraha ya enka.
Majukumu
aliyopewa kiungo huyo ni kumchezesha mshambuliaji wa timu hiyo, Geilson Santos
Santana ‘Jaja’ ili apate nafasi ya kufunga.
Tayari
Maximo amembadilisha namba Coutinho kutoka kiungo mshambuliaji wa pembeni namba
11 na kumtumia kuwa mshambuliaji wa pili, namba 10.
Awali,
kocha huyo alikuwa akimtumia kiungo mshambuliaji mwenye kasi, Mrisho Ngassa
kucheza namba 10 kuanzia mechi za kirafiki na baadhi za ligi kuu.
“Ni
maboresho tu niliyoyafanya kwenye kikosi, kila siku ninajaribu kutengeneza
kombisheni tofauti za wachezaji kwenye timu ili tupate matokeo mazuri,” alisema
Maximo.
Aidha,
akizungumzia kumchezesha Coutinho kwa wastani wa dakika 60 katika mechi mbili
zilizopita, Maximo alifunguka: “Nalazimika kumpa dakika 60 kwa sababu bado
hajawa fiti kwa asilimia 100.”
0 COMMENTS:
Post a Comment