Wachezaji
saba wa Yanga waliopo kwenye kambi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars,
inayojiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Benin, wamewekewa ulinzi mkali
pindi wanapokuwa mazoezini kwa kuhofia kuhujumiwa kutokana na kuwa wiki ijayo
watakuwa na kibarua kikubwa cha kuikabili Simba.
Taarifa
za uhakika kutoka ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) zinasema kuwa
awali uongozi wa Yanga uliwawekea ngumu wachezaji hao kujiunga na timu hiyo,
sababu ikiwa ni hiyohiyo, lakini licha ya kuwaruhusu umetaka wachezaji wao
walindwe na kuwe na uangalizi wa karibu kutokana na hofu hiyo ya pambano la
watani
Kwenye
mazoezi ya Stars, jana asubuhi katika Viwanja vya Gymkhana jijini Dar, ambapo
lilishuhudia ulinzi mkali kiasi kwamba waandishi wa habari walizuiwa kusogelea
kwenye uwanja wa mazoezi mpaka walipopata ruhusa kutoka kwa uongozi.
“Wanawapa
ulinzi mkali sana, wanahofia mechi yao ya Simba na hiyo ndiyo sababu kubwa,”
kilisema chanzo kutoka kwenye kambi ya timu hiyo ya taifa.
Wachezaji
wa Yanga waliopo Stars ni Deogratius Munishi ‘Dida’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’,
Edward Charles, Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Mrisho Ngassa na Simon Msuva.
0 COMMENTS:
Post a Comment