Mbeya City wamezidi kupiga hatua kwenye vitu kadhaa ambavyo vingeweza kufanywa na klabu kongwe za Yanga na Simba.
Sasa wamekuwa wakivifanya wao kama vile utaratibu wa kuuza jezi ambao unaiwezesha klabu kuingiza fedha nyingi.
Safari hii wametengeneza bahasha ambazo zina nembo ya klabu na mdhamini wao mkuu.
Huenda hii inaweza isiwe ni biashara au faida, lakini ni sehemu ya kuonyesha kiasi gani wanaidhamini taasisi yao.
Si taasisi za kiserikali au binafsi nje ya mpira ndiyo zinaweza kufanya hivyo pekee. Hata Mbeya City.







0 COMMENTS:
Post a Comment