October 9, 2014

PAZI (KUSHOTO) AKIWA MAZOEZINI PAMOJA NA MAKIPA, IVO MAPUNDA NA CASILLAS.

Kundi la kwanza la kikosi cha Simba limeondoka nchini na tayari limetua jijini Johannesburg, Afrika Kusini kwa ajili ya kuweka kambi.

Kikosi hicho kinaondoka kwa mafungu, fungu la kwanza likianza jana usiku kwa ndege ya Fast Jet kutokana na wachezaji wengine kuwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa kucheza dhidi ya Benin.

Simba inaweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya mechi yake ya Oktoba 18 dhidi ya watani wake wa jadi Yanga, lakini limeondoka na kumuacha kocha wake wa makipa Iddi Pazi.
Pazi amethibitisha kwamba hatakuwa katika safari hiyo, lakini akataka viongozi ndiyo walizungumzie hilo.
“Kweli mimi nimebaki, nimeambiwa sitakwenda. Sijajua hasa sababu ni nini, uongozi ndiyo unaweza kujibu,” alisema.
Hata alipoulizwa hasa sababu ya msingi au aliomba kubaki, Pazi alisema. “Kwa kweli hata mimi sijui, timu imeamua kujiandaa bila kocha wa makipa.
“Naona si kitu cha kawaida, lakini viongozi wanapaswa kuzungumza kuhusiana na hili, naamini wao watakuwa na jibu.”

Simba imeanza ligi kwa sare tatu mfululizo na mechi dhidi ya Yanga itakuwa ni ya nne, watani wao hao walianza na kipigo lakini wakafanikiwa kushinda mechi zao mbili zlizofuatia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic