October 23, 2014


Simba imetua mjini Mbeya tayari kwa ajili ya mechi yake ya keshokutwa dhidi ya Prisons na leo imefanya mazoezi jioni.

Simba itakipiga na Prisons Jumamosi katika mechi ya Ligi Kuu Bara.
Wekundu hao, wamefanya mazoezi leo jioni na Kocha Mkuu, Patrick Phiri amesema ana imani kikosi chake kitabadili mambo.
"Tunaendelea vizuri, mazoezi yamekwenda vizuri na nina matumaini makubwa tutabadili hali ya sasa," alisema.
Simba imekwenda sare nne mfululizo, zote ikiwa nyumbani Dar es Salaam.
Tayari Kocha Mkuu wa Pirosons, David Mwamwaja ameishawakaribisha Simba na kuwaambia Mbeya, hakuna mchekea.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic