October 12, 2014


Taifa Stars imeitungua Benin kwa mabao 4-0 katika mechi ya kitarafiki ya kimataifa iliyochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Stars yalifungwa na wachezaji wake wawili wanaokipiga nchini na wawili wanaocheza nje ya Tanzania.
Nadir Ali Harob ‘Cannavaro’ wa Yanga ndiye alianza kabla ya Amri Kiemba wa Simba kuongeza la pili.
Mabao mengine mawili yalifungwa na na Thomas Ulimwengu kutoka TP Mazembe na Juma Luizio anayekipiga Zesco ya Zambia.

Stars ilionyesha kiwango kizuri na kuwazidi ujanja Benin katika tarehe hiyo inayotambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimaitaifa.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic