October 8, 2014

RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limepuuza agizo la Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia la kusitisha suala la kuchukua fedha za klabu 14 za Ligi Kuu Bara na kukutana na Bodi ya Ligi.

Badala yake, shirikisho hilo limeendelea kupambana baada ya kumshitaki mwanasheria wa klabu hizo za Ligi Kuu Bara, Dk Damas Ndumbaro kwenye kamati ya Nidhamu ya TFF.
Taarifa zinaeleza, Dk Ndumbaro ametakiwa kufika kwenye kamati hiyo kesho ili kujibu tuhuma za yale aliyozungumza kwenye vyombo vya habari.
Alichokizungumza Dk Ndumbaro ilikuwa ni kupinga TFF kuzikata asilimia 5 klabu hizo kwenye fedha zao za udhamini.
Kama Waziri Nkamia ameagiza wakutane Jumamosi halafu warudi serikali, halafu TFF imeamua kumshitaki mmoja wa waliokuwa wakipinga ‘move’ yao ya kuzidhulumu klabu, maana yake imepuuza agizo hilo.
Taarifaz a uhakika zinasema tayari Dk Ndumbaro ameishapelekewa barua kutoka TFF ikimtaka kuhudhuria kikao cha kamati ya nidhamu kitakachofanyika mchana wa kesho.

Blogu Hii inaendelea kufanya juhudi kumpata Dk Ndumbaro kuhusiana na suala hilo ambalo lilionekana baada ya serikali kuingilia kati kungekuwa na mwanga, lakini TFF imeonyesha jeuri yake.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic