| KIKOSI CHA COASTAL UNION MSIMU ULIOPITA. |
Taarifa kutoka Tanga zimeeleza, uongozi wa Coastal Union umeamua kufanya hivyo kwa madai Bin Slum Tyres waliokuwa wafadhiri wake msimu uliopita wanatengeneza jezi za Coastal Union zikiwa na mdhamini wa Sound.
"Unajua mimi si msemaji, lakini uongozi umekaa juzi na kufikia uamuzi huo kwa kuwa wanaona Bin Slum anatengeneza hizo jezi.
"Lakini hakuna uhakika na hilo, ndiyo maana makubaliano ni kwamba lazima lifanyiwe uchunguzi na kama tukijua kweli, basi tutakwenda mahamani," kilieleza chanzo.
Sound ni aina ya pikipiki na msimu uliopita ilikuwa inavaliwa na Coastak Union kabla ya pande hizo mbili kuhitilafiana.
Sasa Coastal unadhaminiwa na kampuni ya unga ya Pembe.
Juhudi zinaendelea ili kumpata mhusika kutoka kampuni ya Bin Slum Tyres ili awe kufafanua hilo.







0 COMMENTS:
Post a Comment