Kiungo wa Yanga, Emerson Roque na mshambulia
mpya wa Simba, Danny Sserunkuma raia wa Uganda wakatakutana siku ya mechi ya
Bonanza la Mtani Jembe kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Yanga ilimzuia Emerson raia wa Brazil
kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Express, jana. Lakini Simba nayo imemuweka
jukwaani Sserunkuma leo wakati inapambana na Mtibwa Sugar katika mechi ya
kirafiki ndani ya Dimba la Chamazi jijini Dar.
Maana yake wawili hao watakutana katika
mechi hiyo ya kirafiki.
Kuna uwezekano mkubwa wa kupambana kwa kuwa
Sserunkuma ni ‘mtamu’ zaidi anapocheza namba kumi.
Wakati Emerson ameonekana kuwa anatulia
zaidi akicheza kiungo mkabaji, yaani namba sita.
Kutokana na namba zao, maana yake wawili hao
watapambana vilivyo siku hiyo.
Mechi hiyo inasubiriwa kwa hamu kwa kuwa
kila upande una wachezaji kadhaa wapya na tayari Makocha Marcio Maximo na
Patrick Phiri wamekutana mara moja msimu huu na matokeo yakawa suluhu.







0 COMMENTS:
Post a Comment