Manchester United imeendelea kuondoa gundu baada ya kushinda mechi ya nne mfululizo kwa kuichapa Stoke City mabao 2-1.
Ikiwa nyumbani, Manchester United ililazimika kufanya kazi ya ziada hadi ilipopata bao katika dakika ya 21 kupitia Marouane Fellaini.
Licha ya kuwa ugenini Old Trafforfd, Stoke City walikomaa na kusawazisha dakika ya 39 kupitia Steven Nzonzi. Mabao hayo yalidumu kipindi chote cha kwanza.
Kipindi cha pili, Juan Mata ndiye alifunga bao katika ya 59 baada ya kupiga mpira wa adhabu ndogo uliojaa wavuni moja kwa moja.
Hata hivyo, mara kadhaa, beki Marcos Rojo alikuwa akionyesha kidole kwamba aliugusa kabla ya kujaa wavuni.
MATOKEO MENGINE YA LIGI KUU ENGLAND HAYA HAPA:
Burnley 1-1 Newcastle
Swansea 2-0 QPR
C. Palace 1-0 A. Villa
Wes Brom 1-2 West Ham
0 COMMENTS:
Post a Comment