Kocha maarufu nchini, Abdallah ‘King’ Kibadeni amezushiwa kifo na
kusababisha utata mkubwa.
Taarifa ziliripotiwa na mtandao mmoja zimefanya watu waanze
kumpigia simu kila mara.
“Kweli hata mimi napigiwa simu na watu wengi sana kama nimefariki
dunia, hawa watu sijui wamepata wapi hizi taarifa.
“Kweli siku chache zilizopita nimefanyiwa upasuaji wa jicho. Hadi
sasa niko safi kabisa, ninaendesha hata gari.
“Kupitia mtandao wako, naomba niseme hivi; ninawaomba radhi wote
waliopata usumbufu kutokana na taarifa hizi,” alisema Kibadeni na kuongeza.
“Ila ninaomba wale ambao wanaopata taarifa ni vizuri kuzihakikisha
kuliko kusababisha usumbufu kwa watu.”







0 COMMENTS:
Post a Comment