Kiungo mshambuliaji mpya wa Simba, Omar Mboob, ambaye yupo kwa ajili ya majaribio katika kikosi hicho,
amekabidhiwa jezi namba 28 atayokuwa anaitumia ambapo jezi hiyo ilikuwa
inamilikiwa na kiungo, Amri Kiemba ambaye ametimkia Azam FC.
Mboob raia wa Gambia ameanza mazoezi na kikosi hicho cha Wekundu wa Msimbazi juzi Jumatatu katika Gym
ya Chang’ombe, Dar es Salaam.
Msemaji wa timu hiyo, Humprey Nyasio,
alithibitisha kiungo huyo kukabidhiwa jezi hiyo ambapo alisema atakuwa kwenye
majaribio katika kikosi hicho kwa muda wa wiki mbili.
“Ni kweli Mboob amekabidhiwa jezi ya
zamani ya Kiemba (namba 28) ambapo tunatarajia kuwa naye katika kikosi chetu
kwa takribani wiki ambapo atakuwa anafanya majaribio,” alisema Nyasio.
Kama Mboob akifanikiwa kufuzu
majaribio katika timu hiyo, itawalazimu kumtema mchezaji mmoja wa kimataifa
kutokana na kupita idadi ya wachezaji watano iliyowekwa na Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF).
0 COMMENTS:
Post a Comment