Maisha ya kiungo Mbrazil, Andrey Coutinho
yanahesabika kama saa ya “disco’, ni tik tak, tik tak.
Hali hiyo inatokana na uamuzi wa uongozi wa
Yanga kutaka kuongeza nguvu ya ushambuliaji na kumsajili Amissi Tambwe.
Habari za uhakika zinaeleza tayari Yanga
imezungumza na wakala wa Tambwe, lakini bado hawajafikia mwafaka.
Leo ndiyo siku ya mwisho ya usajili,
unafungwa saa sita kamili.
Lakini Yanga inaona ni wakati mwafaka wa
kumnasa Tambwe amabye aliibuka kuwa mfungaji bora.
Lakini Tambwe, ameachwa na Simba na nafasi
yake amepewa Simon Sserunkuma, raia wa Uganda.
0 COMMENTS:
Post a Comment