December 12, 2018


Na George Mganga

Mlinda Mlango wa klabu ya Yanga, Beno Kakolanya amesema hawezi kuzungumzia chochote juu ya kauli za Kocha wake mkuu, Mwinyi Zahera ambaye alieleza kuwa hafahamu alipo mpaka sasa.

Kakolanya ambaye ameamua kujiengua Yanga kutokana na kudai stahiki zake ikiwemo fedha za mishahara na usajili, amesema yanayozungumzwa na Zahera hawezi kuyatolea neno lolote.

Maneno ya Kakolanya yamekuja baada ya siku kadhaa kupita Kocha Zahera kusema anashindwa kuelewa kwanini Kakolanya ameondoka Yanga bila taarifa na akiwa hajui alipo.

Zahera alifunguka hayo kupitia kikao na waandish wa habari baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi baina ya Yanga na Biashara United kutoka mkoani Mara na kusema hawezi kufikiria kumpigia simu Kakolanya kwani hakumpa taarifa kama anaondoka.

Kipa huyo aliyesajiliwa na Yanga kutoka Tanzania Prisons, amesema yeye anachokijua kuwa bado ni mchezaji wa Yanga na bado ana mkataba na klabu hiyo.

Beno mpaka sasa yupo nje ya kambi ya Yanga akidai pesa zake ambapo amekuwa akikosa programu za Zahera mazoezini ikiwa inaelekea takribani wiki sasa.


14 COMMENTS:

  1. Hakuna mchezaji mkubwa kuliko timu.Mbona Yanga ilimvumilia Kokolanya wakati anasumbuliwa na goti msimu mzima alikuwa benchi anauguza majeraha ya goti ikabidi Yanga wamtumie Rostand.Leo hii anagoma ameshindwa kuvumilia.
    Wengi wamepita Yanga imebaki.

    ReplyDelete
  2. Tatizo maskini akipata matako hulia mbwata

    ReplyDelete
  3. Yanga wamlipe Kakolanya. Hakuna cha uvumilivu. Utafanyaje kazi bila malipo? Kama vipi muacheni aende kwenye chama lake, Simba Sports Club

    ReplyDelete
    Replies
    1. hakuna asiyejua kuwa kakolanya ni mmoja kati ya magolikipa bora hapa tanzania.....lakini bahati mbaya yake ni kuwa yanga haina kawaida ya kubembeleza mchezaji......kocha mwinyi zahera ndo kabisaaaa.....na kwa kauli nilizozisikia mwinyi zahera akizitoa mbele ya waandishi wa habari,namshauri mdogo wangu kakolanya atafute tu timu ya kwenda kuitumikia ktk kipindi hiki cha dirisha dogo,vinginevyo akirudi yanga ataozea benchi.....mwinyi zahera hana staa ktk kikosi chake,kila mtu yuko sawa na mwenzake na anaweza akapata namba.....cha muhimu ni kijituma mazoezini na nidhamu.

      Delete
    2. Upo sahihi na ninakuunga mkono 100%

      Delete
    3. Wewe unayesema yanga imwachie aende ktk chama lake simba kwani kazuiliwa tena achangamke maana leo saa sita usiku dirisha linafungwa

      Delete
    4. Who is kakolanya bhana, binafsi niliamini ana kiwango kikubwa Aisha lkn si muungwana Acha tu nae ajifunze.

      Delete
  4. Hakuna mtu mkubwa kuizidi timu. Timu ni mjumuiko wa watu wengi sana. Mtu mmoja hapaswi kuchafua hali ya hewa ya timu nzima. Mi namshauri kama ameahidiwa sehem aende tu na Yanga itaendelea kuwepo.

    ReplyDelete
  5. By THOMAS NG'ITU
    Dar es Salaam. Kumeibuka maneno mengi baada ya kipa Beno Kakolanya kugoma kujiunga na wachezaji wenzake katika kikosi cha Yanga.

    Kakolanya tangu atoke katika kikosi cha timu ya Taifa kilichotoka kucheza mechi dhidi ya Lesotho, hakurejea kwenye klabu yake kwa kile kinachotajwa kudai fedha yake ya usajili.

    Hata hivyo inatajwa kwamba mara kwa mara alikuwa akiwakumbusha mabosi wake kuhusu kulipwa, lakini mabosi hao walikuwa wakimpotezea.

    Mwanaspoti limeangazia baadhi ya vitu ambavyo Kakolanya alijitolea kwenye klabu hiyo licha ya kwamba alikuwa na madai yake.



    KUCHEZA ANAUMWA

    Msimu uliopita kipa Youthe Rostand aligoma kusafiri na timu kwenda mkoani Mbeya kucheza na Tanzania Prisons.

    Kakolanya aliyekuwa majeruhi ya goti, alienda katika timu hiyo ili akae benchi tu, lakini alikutana na kisanga hicho na kujikuta akisafiri kama golikipa pekee.

    Ilimlazimu kucheza huku akiwa na maumivu ya goti, akiwa anadai mishahara na pesa yake ya usajili lakini kwa mazingira yake aliona bora akae golini na kuisaidia timu yake, lakini leo uongozi wa Yanga umesahau kabisa.

    Kama angekuwa na utovu wa nidhamu au jeuri angegoma kipindi kile, lakini Kakolanya alipambana lakini leo hii inabidi tutambue kwamba na yeye ni binadamu labda kapatwa na tatizo kubwa kwanini agome hivi sasa akiwa mzima na sio mwanzo alipopewa mechi huku anaumwa.

    KUIPA YANGA UBINGWA

    Msimu wa mwaka juzi alisajiliwa akitokea katika klabu ya Prisons, usajili ambao pia alihusishwa kujiunga na Simba, lakini akatua Yanga.



    katika msimu huu kwenye mechi 5 za mwisho aliipambania Yanga akiwa golini mpaka wanafanikiwa kuchukua ubingwa.

    Leo hii kisa kagoma wameanza kusema kwamba meneja wake ni Simba basi amegoma ili asajiliwe Simba, wakati huo huo wanasahau Kakolanya huyu alisaini Yanga na meneja huyo huyo na akainyima Simba ubingwa mwaka juzi.

    MICHOMO YA SIMBA NA YANGA

    Baada ya mechi ya Yanga dhidi ya Biashara kocha Mwinyi Zahera alifunguka anashangaa kuona meneja wa Beno ni mjumbe wa Simba.

    Watu wa karibu na kocha huyo wanamlisha maneno sio kwa sababu Kakolanya huyu ambaye alidaka mechi dhidi ya Simba meneja wake ni huyo huyo mjumbe wa Simba.

    Kama ingekuwa anafuata kauli za meneja wake asigeokoa michomo katika pambano hili, hivyo kudai kwake pesa kusiwafanye viongozi wa Yanga kusingizia mambo ya nje ya uwanja kwa kipa huyu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwan Beno ndiyo aliyeipa ubingwa yanga 2017/2017? Alidaka mechi ngapi?

      Delete
    2. Zitafute record vizuri katika mkataba wake wa miaka miwili iloyoisha ameidakia yanga mechi ngapi? Lakini alivumiliwa ukumbuke huu mkataba mpya wakati yanga ipo hoi ndio alete mbwembwe aende tu...ushauri wangu kwake aende jangwani aombe radhi kwa kocha ayajue makosa yake na kuyakiri then maisha yaendelee au awe jiwe aemde ktk timu ya wakala wake maana isije kuwa anatumika kugoma ili yanga iwe dhaifu ipoteze mechi za mikoani na hizo ndio hisia za kocha. Tukubali tu timing ya beno kugoma haikuwa sahihi

      Delete
  6. Kikubwa wayamalize
    Ila DOA limekuja kuwa Meneja wake ni simba. Kwa sasa imani kwake kwa wananchi utakuwa imepungua aiseee.

    ReplyDelete
  7. Dawa ya deni kulipa, maneno maneno ya nini kwa anaekudai?????acheni uswahiliswahili mlipeni haki yake masuala ya nani anadai lakini anacheza hayamuhusu Kakolanya...Kwa hiyo kama fulani hadai na mimi nisidai??Kakolanya sio wa mkumbomkumbo yeye anasimama kama yeye alipwe hakuna namna hapo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic