December 2, 2014

MASAU BWIRE (WA PILI KULIA), AKIJADILI JAMBO NA WAHARIRI WA GAZETI LA CHAMPIONI. MHARIRI KIONGOZI WA CHAMPIONI, SALEH ALLY, PHILIP NKINI NA SHABANI MBEGU.

Msemaji wa klabu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire amefanya ziara ya kutembelea katika ofisi za gazeti la Championi.

Masau amefanya ziara hiyo ambayo alipata nafasi ya kuzungumza na waandishi, wahariri na Mhariri Kiongozi wa Championi, Saleh Ally.
AKISALIMIANA NA MHARIRI WA CHAMPIONI IJUMAA, JOHN JOSEPH (KULIA) KATIKATI NI SHABANI MBEGU, MHARIRI WA CHAMPIONI JUMAMOSI.

Akiwa katika Ofisi za Global Plushers ambao ndiyo wamiliki wa Championi, Bamaga jijini Dar es Salaam, Masau alieleza kufurahishwa na utendaji na ushirikiano kutoka kwa timu ya Championi.

"Pia ni agzeti linalojali timu zote, si Simba au Yanga pekee. Waandishi wa Championi nawasiliana nao sana, mara nyingi wanapenda kujua mambo.
AKIJADILI JAMBO NA OSCAR NDAUKA, MMOJA WA WAHARIRI WAKUU GLOBAL PUBLISHERS.

"Hivyo nashukuru kwa kuwa hapa na uungwana pia wa kunikaribisha, ninaahidi tutaendelea kushirikiana," alisema.
Masau ambaye kitaaluma ni mwandishi, pia mwalimu amekuwa mmoja wa wasemaji maarufu zaidi nchini na hasa katika mchezo wa soka. 


MASAU AKISALIMIANA NA MWANDISHI MWANAMIZI WA CHAMPIONI, WILBERT MOLANDI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic