MANDAWA (KUSHOTO) AKIWA NA WACHEZAJI WENZAKE WA KAGERA SUGAR |
Mshambuliaji
wa timu ya Kagera Sugar, Rashid Mandawa ya mkoani Kagera amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kwa mwezi Novemba mwaka huu ambapo atazawadiwa kitita
cha sh. milioni moja.
Mandawa
ambaye kwa mwezi huo alichuana kwa karibu na mshambuliaji Fulgence Maganda wa
Mgambo Shooting ya Tanga na nahodha wa Simba, Joseph Owino atakabidhiwa zawadi
yake na wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom.
Hafla
ya kukabidhi zawadi hiyo inatarajiwa kufanyika wakati wa mechi ya raundi ya
nane ya ligi hiyo kati ya Simba na Kagera Sugar itakayochezwa Desemba 26 mwaka
huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment