Simba imeendelea kuweka rekodi kwa kuwa timu
ya kwanza kutwaa makombe yanayoanzishwa.
Jana Simba imebeba Kombe la Nani Mtani Jembe
kwa mara ya pili, ikiendelea kushikilia rekodi ya kulibaeba kwa mara ya pili
mfululizo lakini ndiyo ya kwanza kulibeba mwaka jana lilipoanzishwa.
Simba ilikuwa ya kwanza kubeba ubingwa wa
Ligi Kuu Tanzania Bara ilipoanzishwa kwa mara ya kwanza.
Simba wakati huo ikijulikana kama Sunderland
ilibeba ubingwa huo mwaka 1965, ikiwa ni mara ya kwanza kuanzishwa kwa ligi
hiyo ikiwa imelenga kuipatia Tanzania mwakilishi kwenye Kombe la Ligi ya
Mabingwa Afrika.
Ligi ilianzishwa ikiwa ni siku chache baada
ya Rais wa Ghana, Kwame Nkurumah, kutoa kombe lililoanza kugombewa na klabu
bingwa za Afrika.
Halafu Simba ikabeba Kombe la Cecafa kwa
mara ya kwanza lilipoanzishwa tu mwaka 1974.
Lakini jana, imechukua ubingwa wa
0 COMMENTS:
Post a Comment