December 13, 2014

MAYWEATHER
Hatimaye, lile pambano lililokuwa likisubiriwa kwa hamu kubwa limewadia.
Bondia ambaye hajawahi kupoteza hata pambano moja, Floyd Mayweather Jnr amethibitisha kwamba yuko tayari kuzichapa na Manny Pacquiao.

PACQUIAO (KULIA)...

Kama hiyo haitoshi, Mayweather ametamka wazi kuwa pambano hilo litakuwa Mei 2, mwakani.
Imeelezwa kiasi cha chini cha gharama kwa pambano hilo kinatarajiwa kuwa pauni milioni 300, na litakuwa ghali zaidi kuliko yote duniani.
Limekuwa likisubiriwa kwa hamu huku kila mmoja akitamba mwenzake anamhofia.

Sasa Mei 2 mwakani, siku ya kumaliza ubishi wa wababe hao wa masumbwi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic