December 14, 2014


Shabiki mmoja wa Yanga, mwanadada alishindwa kujizuia na kujikuta akimwaga machozi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Saalam.

Dada huyo aliyekuwa kwenye jukwaa la VIP, alimwaga chozi kila muda ulivyokuwa ukisonga katika mechi ya Nani Mtani Jembe wakati Simba ikiongoza kwa bao moja.
Simba ilipopata bao la pili, dada huyo aliendelea kulia. Licha ya kuonyesha anataka kujikaza, alishindwa kujizuia.
Dakika ya 80, aliamua kuondoka zake uwanjani hapo kuonyesha ameshindwa kabisa kuvumilia huku baadhi ya mashabiki wakionyesha kumuonea huruma.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic